Utangulizi
Karibu kwenye Upatu, Application (App) iliyotengenezwa na Jiongeze Fintech Company Ltd (Jiongeze). Upatu ni App ya simu inayokuwezesha
kushiriki michezo ya Upatu kwa uwazi, mpangilio mzuri, na bila gharama yoyote (BURE). Inapatikana kwa watumiaji wa simu za vya Android na iOS.
2. Matumizi ya Application
- App ya Upatu inatumiwa na Viongozi wa Upatu (Kijumbe) na Wachangiji kusimamia michezo yao yote katika App
moja.
- Watumiaji wanaruhusiwa kujiandikisha, kuunda, na kusimamia Michezo ya Upatu.
- App hii ni bure kwa watumiaji wote.
3. Wajibu wa Mtumiaji
- Watumiaji wanapaswa kutoa taarifa sahihi na kamili wakati wa usajili.
- Viongozi wa Upatu (Kijumbe) wanawajibika kusimamia michezo kwa uwazi na kufuata makubaliano na wanachama wao.
- Wachangiaji wanapaswa kushiriki michezo ya Upatu kwa uaminifu na kulipa michango yao kwa wakati.
- Watumiaji wanatakiwa kutumia programu hii kwa madhumuni halali tu.
4. Faragha ya Taarifa
-
Jiongeze inaheshimu faragha ya watumiaji wake. Taarifa zote za watumiaji zitahifadhiwa kwa
usalama na hazitasambazwa kwa watu wengine bila idhini ya mtumiaji.
-
Watumiaji atapata namba ya siri mpya kila atakapoingia kwenye App. Hivyo mtumiaji hapaswi kugawa namba za siri kwa watu wengine.
5. Wajibu wa Jiongeze
- Kuhakikisha kuwa App inafanya kazi kwa ufanisi kwa watumiaji.
- Kutoa usaidizi wa kiufundi pale inapohitajika.
- Kulinda taarifa za watumiaji kwa kuzingatia sera za faragha.
6. Maswala ya Kiufundi
- App ya Upatu inaweza kupatikana muda wote, lakini kunaweza kuwa na changamoto za kiufundi zisizotarajiwa.
- Watumiaji wanashauriwa kuwa na intaneti katika vifaa vyao ili kuweza kutumia App.
7. Haki Miliki
Application ya Upatu ni mali ya Jiongeze Fintech Company Ltd. Watumiaji hawana haki ya kurekebisha au kunakili Application hii bila idhini ya maandishi kutoka Jiongeze.
8. Mabadiliko ya Masharti
Jiongeze ina haki ya kufanya mabadiliko ya masharti haya wakati wowote. Watumiaji watapewa taarifa juu ya mabadiliko hayo kupitia programu au namba za simu.
9. Kuvunja Masharti
Jiongeze ina haki ya kusimamisha au kufuta akaunti yoyote itakayovunja masharti haya yamatumizi.
10. Sheria na Usuluhishi
- Masharti haya yanasimamiwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Migogoro yoyote itatatuliwa kwa mazungumzo au kufikishwa kwenye mamlaka husika za kisheria.
11. Mawasiliano
Kwa msaada au maswali yoyote kuhusu Application ya Upatu, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
- Barua pepe: mchezo@upatu.co.tz
- Simu: +255 685 833 429
- Mitandao ya kijamii (Facebook | Instagram | X | Tiktok: @UpatuApp
Kwa kutumia Application ya Upatu, unakubaliana na masharti haya yote.