1. Utangulizi
Sera hii ya Faragha na Ulinzi wa Data inaeleza jinsi Jiongeze Fintech Company Limited (“sisi,” “Upatu,” au “Jiongeze”)
inavyokusanya, kutumia, kuhifadhi, na kulinda taarifa zako za kibinafsi unapotumia Application ya Upatu. Tunajitahidi
kulinda faragha ya taarifa zako kwa mujibu wa sheria na kanuni za faragha za Tanzania.
2. Taarifa Tunazozikusanya
Tunapokusanya taarifa zako, tunahakikisha kuwa ni kwa madhumuni halali pekee. Taarifa zinazokusanywa ni pamoja na:
- Taarifa za Usajili: Jina na namba ya simu
- Taarifa za Matumizi: Maelezo ya michezo ya Upatu unayounda au kushiriki.
- Taarifa za kifaa: Aina ya kifaa chako, mfumo wa uendeshaji (Android/iOS), na anwani ya IP.
- Taarifa za Mawasiliano: Mawasiliano yako na huduma yetu ya wateja.
3. Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako
Taarifa zako zitakuwa zikitumika kwa madhumuni yafuatayo:
- Kutoa huduma za programu ya Upatu kwa ufanisi.
- Kuwezesha usajili na utumiaji wa programu kwa watumiaji wote.
- Kuboresha huduma na uzoefu wa mtumiaji.
- Kuhakikisha usalama wa michezo ya Upatu na akaunti za watumiaji.
- Kuwasiliana nawe kuhusu masasisho, matangazo, au huduma za ziada.
- Utatuzi wa changamoto za kiufundi au msaada wa huduma kwa wateja.
4. Uhifadhi wa Taarifa
- Taarifa zako zitahifadhiwa kwa njia salama na kulindwa dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa.
- Tunahifadhi taarifa hizi kwa kipindi kinachohitajika kutoa huduma zetu na kutimiza majukumu ya kisheria.
- Taarifa yoyote ya mtumiaji haitahifadhiwa zaidi ya kipindi kinachotakiwa kisheria.
5. Ulinzi wa Taarifa
Tunachukua hatua zifuatazo kulinda taarifa zako za kibinafsi:
- Kutumia teknolojia za usimbaji (encryption) kulinda data zinazosafirishwa.
- Kutumia teknolojia za usimbaji (encryption) kulinda data zinazosafirishwa.
- Kudhibiti upatikanaji wa taarifa kwa wafanyakazi walioteuliwa pekee.
- Kuchukua hatua za kiusalama ili kuzuia uvujaji wa taarifa au udukuzi.
6. Kugawa/Kusambaza Taarifa
- Hatutauza, kukodisha, au kugawa taarifa zako binafsi kwa watu/taasis nyingine bila idhini yako.
- Tunaweza kutoa taarifa kwa:
- Washirika wetu wa huduma kwa madhumuni ya kiufundi na utoaji wa huduma bora.
- Mamlaka za kisheria au serikali pale ambapo inahitajika kwa mujibu wa sheria.
7. Haki za Mtumiaji
Kama mtumiaji wa Application ya Upatu, una haki zifuatazo:
- Haki ya Upatikanaji: Kupata taarifa kuhusu jinsi tunavyotumia data zako.
- Haki ya Marekebisho: Kufanya marekebisho ya taarifa zako zisizo sahihi.
- Haki ya Kufuta Taarifa: Kuomba kufutwa kwa taarifa zako iwapo hazihitajiki tena.
- Haki ya Kuzuia Matumizi: Kukataa matumizi yasiyofaa ya taarifa zako.
8. Cookies
Upatu inaweza kutumia Cookies au teknolojia nyingine zinazofanana ili kuboresha huduma zetu, kutambua vifaa, na
kufuatilia matumizi ya Application. Unaweza kuzima cookies kupitia mipangilio ya kifaa chako.
9. Madiliko ya Sera hii
Jiongeze ina haki ya kubadilisha sera hii mara kwa mara ili kuboresha na kulinda usalama wa taarifa binafsi za watumiaji wa Upatu App. Mabadiliko yoyote yatajulishwa kupitia Application au simu.
Tunaomba upitie sera hii mara kwa mara kuhakikisha unaelewa masharti mapya.
10. Mawasiliano
Kwa maswali au maoni kuhusu Sera ya Faragha na Ulinzi wa Data, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
- Barua pepe: mchezo@upatu.co.tz
- WhatsApp: +255 685 833 429
- Mitandao ya kijamii (Facebook | Instagram | X | Tiktok: @UpatuApp
Kwa kutumia programu ya Upatu, unakubaliana na masharti ya Sera hii ya Faragha na Ulinzi wa Taarifa.